Friday, January 14, 2011

TFF YALAMBA MATAPISHI YAKUBULI MECHI ZA KIRAFIKI ZICHEZWE

MSEMAJI WA TFF WAMBURA.
Shirikisho la kandanda hapa nchini TFF limelegeza msimamo wake kuhusu wa kutoruhusu mechi za kimataifa za kirafiki  kwa vilabu vya ligi kuu vikiwemo vya SIMBA na YANGA.

Msemaji wa TFF, BONIFACE WAMBURA anasema wamekutana na viongozi wa chama cha soka mkoa wa DSM DRFA ambao ni moja ya waratibu za mechi hizo na wamekubaliana sasa kwamba  mechi za kimataifa za kirafiki kwa SIMBA na YANGA dhidi ya klabu ya soka ya ZESCO ya ZAMBIA na  na ile ATLETICO PARANAENSE ya BRAZIL zitachezwa.

klabu ya soka ya ATLETICO PARANAENSE ya BRAZIL ipo kwenye nafasi ya TANO ya msimamo wa ligi kuu ya nchi hiyo ikiwa na pointi SITINI, na nikukumbushe pia kwamba ligi hiyo inaongozwa na klabu ya FLUMINENSE yenye pointi 71 ikifuatiwa na CRUZEIRO, halafu nafasi ya tatu ipo CORINTHIANS na GREMIO katika nafasi ya nne.

SIMBA  wanarejea DSM na watacheza na klabu ya ZESCO ya ZAMBIA na watatumia mechi hiyo kuwaonesha mashabiki wao kombe la MAPINDUZI  waliloshinda siku mbili zilizopita huko ZANZIBAR. 

Siku ya Jumapili itakuwa zamu ya YANGA kucheza na ZESCO kwenye dimba la UHURU.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU