Monday, February 7, 2011

SAFARI LAGER ,NYAMA CHOMA YAZINDULIWA

Kampuni ya bia nchini TBL kupitia bia yake ya SAFARI LAGER imezindua mashindano ya kuchoma nyama ambayo fainali zake zinatarajia kufanyika MACHI 27 mwaka huu ambapo washindi wa tano wataingia fainali huku bingwa akiibuka na shilingili milioni moja.
Meneja wa bia ya SAFARI LAGER ambao ndio wadhamini wa shindano hilo FIMBO BUTALLA amesema kuwa shindano hilo linatarajia kuleta ushindi mkubwa kwa washiriki na kuboresha katika huduma yao .
BUTALLA amesema mshindi wa pili atapata shilingi laki nane,mshindi wa tatu  laki sita, mshindi wa nne  laki nne huku mshidni wa tano akiibuka na kitita cha laki mbili.
Shindano hilo linatarajia kufanyika katika mikao ya DSM,MBEYA KILIMANJARO na ARUSHA Utaratibu wa kupata baa zitakashiriki mashindano haya utaendeshwa kwa njia ya simu,ambapo wananchi watatakiwa kutuma ujumbe usemao SAFARI KISHA MKOA UILIOPO IKIFUATIWA NA JINA LA BAA KISHA TUMA KWENDA NAMBA 15540.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU