Monday, February 7, 2011

BMT INASUBIRI UTEKELEZAJI WA CHANETA NA CHANEZA BAADA YA KUMALIZA MGOGORO WAO



Baraza la michezo nchini BMT limevitaka vyama vya netiboli TANZANIA BARA na VISIWANI kutekeleza makaubaliano yao kama walivyokubaliana wakati wa kuondoa tofauti zao na si kurudi nyuma tena

Baada ya marumbano ya muda mrefu baina ya Chama cha netiboli Bara  na chama cha netiboli visiwani sasa vyama hivyo vilikaa pamoja na kumalizamgogoro wao na kuahidi kushirikiana.

Ni wiki moja imepita tangu vyama hivyo vilipokaa pamoja na kumaliza mgogoro ambao ulikuwa umeweka mpaka kati ya CHANEZA na CHANETA.

Mgogoro huo umemalizika baada ya kukaa pamoja na kuyashirikisha mabaraza ya mchezo kutoka BARA na VISIWANI ambao walikuwa wasikilizaji.

Katibu mkuu wa Baraza la michezo Taifa BMT HENRY RIHAYA anesema serikali inasubiri kuona utekelezaji wa makubariano yao na si vinginevyo

Mgogoro wa CHANEZA NA CHANETA ulisababisha kutokuwepo kwa mashindano ya muungano pamoja na kutoshirikiana kuandaa timu ya netiboli ya TAIFA inapojiandaa na mashindano ya kimataifa.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU