Tuesday, February 8, 2011

STEPHANO MWASIKA NA NURDIN BAKARI WAKOSA SAFARI YA ETHIOPIA

NURDIN BAKARI MCHEZAJI WA YANGA.

Msemaji wa YANGA LOUIS SENDEU amesema  wachezaji STEPHANO MWASIKA pamoja NURDIN BAKARI hawatakwenda nchini ETHIOPIA kwa ajili ya mchezo wa marudiano na timu ya DEDEBITS kutokana na wachezaji hao kuwa wagonjwa.

Kikosi cha YANGA kinatarajia kuondoka alhamis wiki hii kwenda nchini ETHIOPIA kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kombe la shirikisho ambapo katika mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka sare ya kufungana magoli manne kwa manne,kwa matokeo hayo yanga inahitaji ushindi wa goli moja kwa bila ili kusonga mbele katika mashindano hayo

Katika hatua nyingine shirikisho la sokanchini TFF limesema tayari wachezaji wa yanga ambao walikuwa hawajajiunga na timu ya Taifa Taifa Stars wamejiunga baada yanga kupelekewa barua ya kuwataka wachezaji huo.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU