Kituo cha mazoezi cha GENESIS kilichopo kijitonyama jijini DSM kimeandaaa tamasha la mazoezi ya viungo la wazi litakalofanyika tarehe 5 mwezi huu katika viwanja vya LEADRES CLUB jijini DSM.
Mratibu wa tamasha hilo ambaye ni meneja wa kituo hicho SAMUEL KIHAMPA amesema kuwa tamasha hilo hufanyika kila mwaka ,malengo yake yakiwa ni kuwakutanisha wakazi mbali mbali wa jiji la DSM ambao hufanya mazoezi katika vituo mbali mbali vya mazoezi.
KIHAMPA amesema tamasha hilo litakuwa bure yaani hakuna kiiingilio, na litafanyika kuanzia saa moja asubuhi hadi saa nne na nusu.
Watu mbali mbali wameombwa kuja kwa wingi pamoja na familia zao ili kuweza kufanya mazoezi hayo ambayo ni faida kwa afya zao.
Amesema kuwa katika mazoezi hayo zaidi ya walimu 16 kutoka katika vituo mbali mbali watafundisha kwa muda wa masaa matatu katika staili tofauti tofauti.
Pia amesema tamaha hilo kutakuwa na wataalamu wa afya watakaowapima wanamichezo watakaohudhuria tamasha hilo magonjwa mbali mbali yakiwemo kisukari na presha.
0 maoni:
Post a Comment