Uamuzi wa kujiuzuru umefikiwa katika kikao cha dharura cha kamati ya utendaji cha shirikisho la mpira wa miguu mkoa wa TABORA kilichokutana na kubaini ukiukwaji wa kanuni uliofanywa na katibu wa TAREFA kwa niaba ya Kamati hiyo.
Mara baada ya kikao hiki cha dharura Mwenyekiti wa TAREFA ALHAJI ISMAIL ADEN RAGE akatamka maamuzi yao kuwa kutokana na kutowajibika ipasavyo kamati nzima ya utendaji pamoja na mwenyekiti wameamua kujihuduru.
Wakati uamuzi huu ukifanyika Katibu wa TAREFA ALBERT SITTA hakuwemo ndani, alikuwa ametolewa nje ili ajadiliwe kwa madai ya ukiukwaji wa kanuni za uongozi, lakini alipohojiwa nje akawa tofauti na uamuzi wa viongozi wenzake na kudai kuwa yeye hajajiudhuru.
1 maoni:
Twashukuru kwa kutupa taarifa hii Jane John
Post a Comment