Tuesday, March 1, 2011

KAIJAGE AITUPIA LAWAMA KAMATI KWA KUTOTOA MAAMUZI SAHIHI

Aliyekuwa Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) amesema kamati maalum iliyokuwa ikifanya uchunguzi wa kutopigwa kwa nyimbo za Taifa kwenye Uwanja wa Taifa haikumtendea haki katika kutoa maamuzi hayo

Akizungumza DSM Kaijage amesema kamati hiyo ilitoa taarifa ya uchunguzi wake na kumtuhumu yeye kama muusika mkuu wa kutopigwa kwa wimbo huo.
Amesema  katika vikao malum vya kumuhoji vilikuwa vya watu wawili mwenyekiti na makamu wake hivyo idadi ya wajumbe ilikuwa haijatimia alishangaa mara zote mbili alikuwa akihojiwa na watu wawili pekee wakati kamati hiyo ilikuwa na wajumbe 5 hivyo hata nusu yake walikuwa hawajafikia
Kaijage amesema ikumbukwe kuwa TFF inatambua umuhimu wa ukamilifu wa Wajumbe katika vikao mifano ipo mingi ya kuthibitisha jambo hilo.
Amesema ibara za 46 na 47 za katiba ya TFF inazungumzia kamati za nidhamu na rufaa, ambapo katiba inabainisha wazi kuwa kamati hizo ziweze kufikia uamuzi ni lazima ziwe na wajumbe wasiopungua watano kamati hizo za watu saba.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU