Tuesday, March 1, 2011

VIJANA KUCHEZA NA CAMEROON MACHI 27 BADALA YA MACHI 26

Mchezo  wa timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 23 (U-23) dhidi ya timu ya taifa ya Cameroon utafanyika Machi 27 badala ya 26 mjini Younde kama ilivyopangwa awali.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema taarifa iliyofika kutoka kwenye chama cha mchezo huo nchini Cameroon (CFF), zinasema mchezo huo umesogezwa mbele kwa siku moja.

Wambura amesema kikosi cha wachezaji wa timu hiyo kitaondoka nchini Machi 24 badala ya 22 ambayo ilipangwa hapo awali na benchi la ufundi.

Aidha, ofisa huyo alisema wachezaji waliotakiwa kujiunga na timu hiyo kutoka Zanzibar wamejiunga pamoja na msaidizi wa Julio, Ayoub Mohamed.

Katika hatua nyingine shirikisho la  Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imelaani kitendo cha Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba Swed Nkwabi, kuingia Uwanja wa Uhuru Dar es salaam na Silaha ikiwa ni pamoja na kuwatisha wasimamizi wa mlangoni baada ya kumzuhia kuingia.

 Ofisa habari wa TFF, Boniface wambura, amesema  TFF inapenda kuwakumbusha viongozi na mashabiki wa Mpira wa Miguu nchini kuwa hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia Uwanjani bila tiketi na Silaha.

Amesema hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia Uwanjani na silaha isipokuwa askari polisi ambao huingia viwanjani kwa kazi ya kuhakikisha usalama unakuwepo kwa watu wote.
Alisema TFF innawakubusha viongozi na mashabiki kuwa hakuna anayeruhusiwa kuingia Uwanjani bila tiketi, ndiyo maana TFF kama zilivyo klabu husika hulazimika kuwanunulia tiketi watu wao ambao wanaamini wanastaili kuingia bure Uwanjani .

Nkwabi alifanya kitendo hicho Jumapili wakati wa mchezo wa Simba na Mtibwa Sugar ambapo baada ya mchezo alitakiwa kwenda kutoa maelezo katika kituo cha Polisi Chang'ombe.

Baada ya kuzuiliwa na Walinzi kuingia Uwanjani bure ndipo alipochomoa Bastola yake kiunoni na kufanya watu watimue mbio kujinusuru.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU