Aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu za taifa za vijana, Rodrigo Stocker kutoka nchini Brazil ameamua kuvunja mkataba wake na TFF kutokana na matatizo ya kifamilia.
Msemaji wa TFF Wambura amesema Stockler amefikia uamuzi huo kwa vile baba yake amekuwa mgonjwa kwa muda mrefu anahitaji uangalizi wake wa karibu.
Amesema TFF imekubali ombi la kocha huyo kutokana na sababu alizotoa na kuzingatia kuwa mkataba wake ulikuwa umebakiza miezi miwili kumalizika.TFF inamshukuru kwa kazi aliyoifanya kwa kipindi chote cha mkataba wake alipokuwa nchini kuanzia Mei 2008, akifundisha timu za vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) na chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes).
0 maoni:
Post a Comment