Tuesday, March 1, 2011

KILI MARATHON YATAKIWA KUANZIA NGAZI YA MKOA

Waziri wa Habari ,vijana Utamaduni na Michezo NCHIMBI amewataka waandaji wa mashindano ya KILI MARATHON kuanza kuandaa mashindano ya riadha kuanzia ngazi ya mikoa ili TANZANIA iweze kupata wawakirishi wazuri katika mashindno hayo yanapofikia nganzi ya kimataifa.

NCHIMBI amesema katika mashindano ya MARATHON yaliyo malizika hivi karibuni TANZANIA imeshindwa kufanya vizuri kutokana na maandalizi duni .

Amesema kama waandaaji waweka mkakati wa kuanza chini ngazi ya mkoa ili  mwakani TANZANIA iwakirishwa na wanariadha wenye uwezo kuliko hivi sasa ushindi unakwenda kwa nchi jirani.

Katika mashindano hayo ya MARATHON washindi wa kwanza walitoka KENYA wakati katika mbio za nusu MARATHO mshindi wa kwanza mpaka wa sita walitoka KENYA huku TANZANIA ikishika nafasi ya saba,zaidi ya nchi 36 zilishiriki mashindano hayo ambayo kila mwaka hufanyika mkoani KILIMAJARO .

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU