KLABU ya kuogelea ya DSM imeanza mkakati wa kuhamasisha waogeleaji chipukizi kujifunza mchezo kuanzia umri wa miaka SITA na kuendelea.
Kocha wa mchezo huo katika klabu hiyo FEREK KALENGELA amesema katika kukuza vipaji, tayari baadhi ya waogeleaji chipukizi kuanzia umri wa miaka TISA hadi KUMI na SITA watashiriki katika mashindano ya kimataifa ya ZAMBIA GALA
Pia mwogeleaji mwingine atakayewakilisha nchi katika mashindano hayo, HILAL HILAL ambaye yupo katika kategori ya umri kuanzia miaka KUMI na SITA na kuendelea anasema ana matumaini ya kufanya vizuri katika mashindano hayo kwani mashindano ya ZAMBIA ni ya TATU kwake kimataifa
Timu hiyo inaondoka nchini kesho kwenda ZAMBIA kushiriki mashindano hayo ambayo yanashirikisha nchi nyingine kama MALAWI na ZIMBABWE, MSUMBIJI, GABON na TANZANIA





0 maoni:
Post a Comment