Friday, March 11, 2011

ADOLF RISHAD AWA MENEJA WA TIMU YA VIJANA UNDER 23

Msemaji wa TFF BONIFACE WAMBURA akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa TFF
                            Waandishi wa habari wakimsikiliza msemaji wa TFF WAMBURA.

WAKATI timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 23 ikijiandaa na mchezo wake wa kutafuta tiketi ya kucheza mashindano ya OLYMPIKI ya mwakani nchini UINGEREZA dhidi ya CAMEROOUN, shirikisho la soka nchini (TFF) limeongeza nguvu katika benchi la ufundi kwa kumweka meneja wa timu hiyo ADOLF RISHAD.

Afisa habari wa shirikisho hilo , TFF , BONIFACE WAMBURA mbali na kumuongeza meneja huyo pia kwa sasa zinatafutwa mechi za kirafiki ili kuipima timu hiyo ya vijana inayaotarajia kucheza na CAMEROOUN , MACHI 27 mjini YAOUNDE na baadae kurudia na timu hiyo wiki mbili baade mjini DSM.

TFF inafanya mipango ya kuwasiliana na timu za AZAM FC, MTIBWA SUGAR na timu ya taifa ya UGANDA ya vijana chini ya miaka 23.

Timu ya Vijana ya Tanzania chini ya miaka 23 kwa sasa inaongozwa na kocha JAMHURI KIHWELO JULIO na kocha MOHAMED AYOUB.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU