Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Leodegar Tenga akizungumza
wakati akifunga Mkutano Mkuu wa shirikisho hilo uliofanyika Machi 27 mwaka huu
ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam.
wakati akifunga Mkutano Mkuu wa shirikisho hilo uliofanyika Machi 27 mwaka huu
ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
wakifuatilia hotuba ya Rais wao Leodegar Tenga. Mkutano huo wa mwaka 2010
ulifanyika Machi 27 mwaka huu ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam.
wakifuatilia hotuba ya Rais wao Leodegar Tenga. Mkutano huo wa mwaka 2010
ulifanyika Machi 27 mwaka huu ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam.
YAH: MAAMUZI YA MKUTANO MKUU
28/03/2011
Mkutano mkuu wa kawaida wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ulifanyika kwa siku mbili kwenye Ukumbi wa Water Front jijini Dar es salaam kuanzia Machi 26.
Mkutano huo, ambao ni chombo cha juu cha maamuzi kwenye shirikisho, ulipitisha mapendekezo makubwa matatu;
Kupitisha bajeti ya mwaka 2011 ambayo inaonyesha kuwa matarajio ya makusanyo kutoka vyanzo mbalimbali ni Sh. 6,199,143,120/= na matumizi ya Sh6,128,354,040. Kwa mujibu wa bajeti hiyo kunja nakisi ya Sh.70,789,080 ambayo kimahesabu inaonekana kuwa ni ndogo.
Hata hivyo, kiwango hicho cha mapato hakitoi picha halisi ya fedha zinazotarajiwa kuingia TFF kutokana na masuala ya kiufundi yanayoendana na fedha za udhamini.
Mkutano mkuu pia uliipa ridhaa Kamati ya Utendaji kuanza mchakato wa kuongeza wanachama wapya baada ya serikali kutangaza mikoa mipya minne. Kwa mujibu wa katiba ya TFF, moja ya sifa kuu za kuwa mwanachama wa TFF ni mikoa ya kijiografia ya serikali. Mikoa hiyo mipya iliyotangazwa na serikali ni Simiyu, Geita, Njombe na Katavi.
Mkutano mkuu pia ulipitisha pendekezo la Kamati ya Utendaji la kuunda Kamati Ndogo ya Ligi Kuu ambayo itaundwa kwa lengo la kuendesha Ligi Kuu kwa uhuru.
Mbali na maamuzi hayo mawili, Mkutano Mkuu pia ulijadili kwa kina mpango wa kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni hadi kufikia watatu, lakini suala hilo likaachwa kwa Kamati ya Utendaji kulitengenezea taratibu kabla ya kuanza kutumika msimu wa mwaka 2013/14.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu pia waliipongeza timu ya taifa kwa ushindi wake wa mabao 2-1 dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Katika ambao ni wa Kundi D la mashindano ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Mataifa ya Afrika za mwaka 2012. Kutokana na ushindi huo, wajumbe walikubaliana kuchangia Sh20,000 kila mmoja ili wapewe wachezaji kama zawadi
0 maoni:
Post a Comment