SAM TIMBE na FELIX MINZIRO
Makipa wa YANGA wakiwa hoi kwa mazoezi
Baada ya mazoezi maji
Wachezaji wa YANGA wakiwa mazoezini.
Kocha mkuu wa klabu ya YANGA, SAM TIMBE amewataka wachezaji wake kujituma zaidi katika mazoezi endapo wanataka nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.
wakati wa mazoezi ya YANGA katika viwanja vya KAUNDA jijini DSM, KOCHA TIMBE amesema kwa sasa ameamua kufanya mabadiliko ya kikosi cha kwanza na ameweka mkazo kwa wachezaji wale tu wanaojituma katika mazoezi ya kila siku
Kuhusu mchezo unaofuata dhidi ya AZAM utakaopigwa MACHI 30 jijini DSM, kocha TIMBE ana imani kubwa ya kufanya vema na hatimaye kunyakua ubingwa wa ligi kuu TANZANIA BARA
Klabu ya YANGA pia inakabiliwa na wachezaji majeruhi akiwemo mlinda mlango YAW BERKO, SHAMTE ALLY na ATHUMAN IDD CHUJI, na katika msimamo wa ligi iko nafasi ya pili na alama 40 hivyo iko nyuma ya mahasimu wao wa jadi SIMBA wenye alama 44 kileleni mwa ligi.
0 maoni:
Post a Comment