Tuesday, March 22, 2011

SERIKALI KUTAFUTA WAKALA WA KUENDESHA UWANJA WA TAIFA


Serikali imesema inatafuta uwezekano wa kumtafuta wakala wa ndani ya nchi wa kuendesha uwanja wa taifa baada ya kushindwa kumpata mwendeshaji wa uwanja huo katika mchakato uliofanyika mwaka jana.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, EMMANUEL NCHIMBI ameyasema hayo katika Mkutano wake na Jukwaa la wahariri jijini DSM ambapo amesema nia ya serikali ni kuufanya uwanja huo uwe wa kisasa zaidi

Pia NCHIMBI amesema serikali inatafuta uwezekano wa kupunguza makato ya viingilio ili kuviwezesha vilabu shindani kunufaika zaidi na viingilio hivyo.

Hata hivyo, akaonyeshwa kukerwa na tabia za baadhi ya watu wanaoharibu kwa makusudi baadhi ya samani ndani ya uwanja huo na kusema hiyo siyo tabia ya kizalendo.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU