Tuesday, April 5, 2011

AZAM YAIZIMA POLISI TANZANIA MAGOLI MATATU KWA MOJA


Ligi kuu soka Tanzania bara imeendelea tena  kwa mchezo mmoja tu uliochezwa katika dimba la UHURU jijini DSM.

Katika mchezo huo AZAM FC wakiwa wenyeji wa maafande wa POLISI TANZANIA wameibuka na ushindi wa magoli MATATU kwa MOJA.

JOHN BOCCO ADEBAYOR alifunga bao la kwanza kwa AZAM huku MRISHO NGASSA akimalizia kazi kwa magoli mawili ya ushindi na hivyo kufikisha magoli KUMI NA NNE akiwa kinara wa mabao akimtangulia GAUDENCE MWAIKIMBA wa KAGERA SUGAR kwa goli moja.

Bao la kufutia machozi la POLISI TANZANIA limefungwa na BANTU ADMIN.

Kwa matokeo hayo AZAM FC sasa wamefikisha alama 40 wakiwa bado katika nafasi ya tatu kimsimamo ikiwa ni alama TATU nyuma ya YANGA na alama TANO nyuma ya vinara na mabingwa watetezi SIMBA.

SIMBA wao wanashuka dimbani kesho kuumana na JKT RUVU katika mchezo muhimu wa kuamua hatma ya utetezi wa SIMBA katika taji la ligi kuu Tanzania bara.

SIMBA wanahitaji ushindi tu katika mchezo huo wa kesho ili kuwa na uhakika wa kutetea taji lao huku matokeo yoyote ya sare ama kufungwa yatakuwa yanawaharibia SIMBA na kuwapa nafasi mahasimu zao YANGA kutwaa ubingwa.

YANGA wao wanashuka dimbani siku ya alhamisi kuwakabili AFRICAN LYON.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU