Thursday, April 7, 2011

MAKOCHA WA TANZANIA NA CAMEROON WATAMBIANA KUSHINDA

    Hata uwanjani ikiwa hivyo wakati wa mechi itapendeza sana JULIO akikumbatiana na kocha wa CAMEROON wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za TFF Jiji ni DSM
 JULIO akionyesha uzalendo na kocha wa timu ya CAMEROON
 SHABAN KADO kipa wa U23 pamoja na kocha wa TANZANIA JULIO wakati wa mkutano na waandshi wa habari katika ofisi za TFF
             Kocha wa timu ya CAMEROON pamoja na nahodha katikati pamoja na kiongozi wa timu hiyo.

Makocha wa timu za vijana chini ya umri wa miaka 23 wametambiana kushinda katika mchezo wa kuwania kushiriki mashindano ya OLIMPIKI 

Kocha Jamhuri Kihwelo ameongeza wachezaji saba kwenye kikosi chake cha U23 kwa
lengo la kukiimarisha kabla ya mechi ya marudiano ya michuano ya Olimpiki dhidi
ya Cameroon itakayofanyika Jumamosi (Aprili 9 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.

Wachezaji hao ni Kigi Makasi kutoka Yanga, David Luhende (Kagera Sugar), Jabir
Aziz (Azam), Kelvin Chale (Simba), Ali Lundenga (Kagera Sugar), Mrisho Ngasa
(Azam) na Juma Abdul (Mtibwa Sugar).

Baada ya uamuzi huo wa kocha, baadhi ya washabiki na vyombo vya habari
vimeonesha mashaka juu ya umri wa Ngasa. Kwanza TFF inapenda kuweka wazi kuwa
umri chini ya miaka 23 ndiyo sifa ya msingi ya kuchezea timu hiyo.

Hivyo uamuzi wa kocha kuita wachezaji hao mbali ya vigezo vingine, cha umri pia
kimezingatiwa. Umri wa Ngasa aliyezaliwa Aprili 12, 1989 ni miaka 22. Wachezaji
wengine walioongezwa na tarehe zao za kuzaliwa ni Makasi (Februari 2, 1990),
Luhende (Januari 21, 1989), Aziz (Januari 1, 1989), Chale (Juni 19, 1992),
Lundenga (Septemba 12, 1990) na Abdul (Novemba 10, 1992).

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU