Monday, April 4, 2011

MAONYESHO YA MAVAZI YAMALIZIKA RASMI

Maonyesho ya Harusi ya 2011 yaliyodumu kwa takriban siku tatu mfululizo toka tarehe 1 mpaka 3 mwezi April yamemalizika rasmi jana katika ukumbi wa Diamond Jubilee, huku yakiwa yamefikia malengo kwa asilimia kubwa zaidi ya yale ya mwaka jana.

Akizungumza katika kuhitimisha maonyesho hayo, muaandaaji na muasisi wa maonyesho hayo Mustafa Hassanali alisema kuwa, wamefanikiwa kwa asilimia kubwa kwa yale yote walioyapanga, na kufanya maonyesho ya mwaka huu kuwa na vionjo kadha wa kadha.

“tulipanga mengi kuyafanya katika maonyesho ya Harusi kwa mwaka huu, na mengi hayo yamefanikiwa kwa mwaka huu, hii imetupa faraja ya kuanza kujipanga kwa mwaka ujao. Ni kazi ngumu kuandaa maonyesho makubwa kama haya, ila kwa kuwa tulihitaji kuwaweka pamoja wafanyabiashara na wajasiriamali wa kazi za Harusi, ilibidi tufunge mkanda kukamilisha.”alisema Mustafa Hassanali.

Maonyesho hayo ya Harusi yaliweza kuwakusanya zaidi ya wafanyabiashra 51 walioonyesha bidhaa zao, kupata mtandao wa kibiashara kwa kukutana na afanyabiasharawengine, pia wateja waliokuja kununua na kujionea mambo mbalimbali katika ukumbi huo, bidhaa zilizoonyeshwa katika maonyesho hayo ilikuwa ni pamoja na magauni ya Harusi, mapambo, keki, picha na bidhaa nyingi zizokamilisha Harusi kwa ujumla.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU