Bondia Deo Njiku
Bondia mtanzania DEO NJIKU ameondoka nchini hii leo kuelekea UFILIPINO kwa ajili ya pambano la ubingwa wa DUNIA uzito mwepesi dhidi ya bondia wa huko PANK GONZAYAEL.
wakiongea kabla ya kupanda ndege kuelekea UFILIPINO, mratibu wa pambano hilo kutoka kamisheni ya masumbwi nchini, ANTONY LUTTA amesema huo ni mwendelezo wa kuwatangaza mabondia wa TANZANIA nje ya nchi huku bondia DEO NJIKU akiwa na imani ya kufanya vema na hatimaye kupata mkanda wa kwanza wa DUNIA
BONDIA NJIKU anayetoka mkoa wa MOROGORO katika kambi ya bondia maarufu nchini FRANSIS CHEKA atapanda ulingoni kuumana na GONZAYAEL anayetoka kambi ya bingwa wa DUNIA, MANNY PACQUIAO
Pambano hilo litakalofanyika APRIL TISA jijini MANILA ni la kwanza la kimataifa kwa DEO NJIKU ambaye amepigana mapambano kumi na sita hapa nchini.
0 maoni:
Post a Comment