Tuesday, April 5, 2011
VIINGILIO U23 CHINI KABISA BUKU
VIINGILIO U23 v CAMEROON
Viingilio katika mechi ya marudiano ya mchujo ya michuano ya Olimpiki kati yatimu ya Taifa ya Tanzania ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 23 dhidi yaCameroon itakayochezwa Jumamosi (Aprili 9 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar esSalaam ni kuanzia sh. 1,000.
Mashabiki watakaokaa viti vya kijani, bluu na rangi ya chungwa (orange) ndiyowatakaolipa sh. 1,000 wakati VIP B na VIP C kiingilio kitakuwa sh. 5,000. Jukwaala VIP A lenye viti 745 kiingilio kitakuwa sh. 10,000. Tiketi zitaanza kuuzwasiku moja kabla ya mchezo na siku yenyewe ya mechi.Tiketi zitauzwa katika vituo vya OilCom Ubungo, Shule ya Sekondari BenjaminMkapa, mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Samora/Ohio, Bigbon Msimbazi (Kariakoo)na Uwanja wa Uhuru. Mechi itaanza saa 10 kamili Cameroon imewasili nchini jana saa 5.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways ikiwana wachezaji 23 na imefikia Paradise City Hotel.
FIFA YAISIMAMISHA BOSNIA-HERZEGOVINA
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA) limeisimamisha
Bosnia-Herzegovina kuanzia Aprili Mosi mwaka huu baada ya Mkutano Mkuu wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu la nchi hiyo (FFBH) kutopitisha Katiba yake
iliyofanyiwa marekebisho kwa kuzingatia matakwa ya FIFA na Shirikisho la Mpira
wa Miguu la Ulaya (UEFA).
Kwa mujibu wa barua ya Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke iliyotumwa kwa
wanachama wake, FFBH inapoteza haki zote ilizokuwa nazo kutokana na uanachama
wake kwa Shirikisho hilo hadi hapo itakapotolewa taarifa nyingine.
Kutokana na kusimamishwa huko, wanachama wote wa FIFA hawatakiwi kushirikiana na
FF BH katika masuala yoyote isipokuwa yale yanayohusu mchezaji binafsi. Hatua
hiyo imefikiwa kutoka na uamuzi uliofikiwa Oktoba 28 mwaka jana na Kamati ya
Utendaji ya FIFA kuwa FFBH iwe imetekeleza matakwa hayo kufikia Machi 31 mwaka
huu.
0 maoni:
Post a Comment