Kocha Jamhuri Kihwelo ameongeza wachezaji saba kwenye kikosi chake cha U23 kwaajili ya mechi ya marudiano ya mchujo ya michuano ya Olimpiki dhidi ya Cameroonitakayochezwa Jumamosi (Aprili 9 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji hao ni Kigi Makasi kutoka Yanga, David Luhende (Kagera Sugar), JabirAziz (Azam), Kelvin Chale (Simba), Ali Lundenga (Kagera Sugar), Mrisho Ngasa(Azam) na Juma Abdul (Mtibwa Sugar).
Kwa mujibu wa kocha JULIO anasema kuongezwa kwa wachezaji hao kumetokana na baadhi ya wachezaji waliokuwepo awali kuwa majerehu hivyo imemlazimu kuongeza wachezaji wa kuziba nafasi hizo
0 maoni:
Post a Comment