Katibu wa chama cha soka mkoa wa DSM (DWFA) STEPHANIA KABUMBA akiwa ofisini kwake katika ofisi za TFF.
Chama cha soka la wanawake mkoa wa DSM (DWFA) kimeitaka timu ya MDELA kurudisha kombe la ubingwa walilipata mwaka jana kwani kombe hilo linatakiwa kukabidhiwa kwa timu ya MBURAHATI iliyotwaa ubingwa ligi ya DSM mwaka huu.
Katibu mkuu wa DWFA STEPHANIA KABUMBA amesema kuwa wameiandikia timu hiyo barua ya kuwataka warudishe kombe hilo lakini uongozi umekuwa hatoi majibu
Katibu amesema soka la wanawake haliwezi kuendelea iwapo vilabu vinakuwa nyuma katika kufanikisha maendeleo ya soka.
Timu ambayo inasubiria kukabidhiwa kombe hilo ni timu ya MBURAHATI QUEEN ambayo mpaka sasa hajapewa kutokana na kikombe hicho kuwa mkononi mwa timu ya MDELA.
0 maoni:
Post a Comment