Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23 inatarajia kuondoka nchiniAprili 15 mwaka huu kwenda Kampala, Uganda kwa ajili ya mechi ya mchujo yamichezo ya Afrika (All Africa Games) itakayochezwaJumamosi (Aprili 16 mwaka huu)
Mechi hiyo itakayofanyika Uwanja wa Mandela (Namboole) kuanzia saa 10 kamilijioni itasimamiwa na Kamishna Jean-Didier Masamba Malunga kutoka Jamhuri yaKidemokrasi ya Congo (DRC). Waamuzi ni Nur Adbulle, Salah Abukar na HassanMohamed kutoka Somalia.
U23 itakuwa na msafara wa watu 30 wakiongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA), Hafidh Ally Tahir. Benchi la Ufundilitakuwa na watu sita wakiongozwa na Kocha Mkuu Jamhuri Kihwelo wakati wachezajini 20. Timu inatarajia kurejea Dar es Salaam, Aprili 17 mwaka huu.
Mechi ya marudiano itachezwa Aprili 30 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Michuano ya All Africa Games itafanyika jijiniMaputo,Msumbiji kuanzia Septemba3-18 mwaka huu.
Timu zimepangwa katika Kanda Saba ambapo mshindi wa kila kanda pamoja namwenyeji Msumbiji ndiye atakayekwenda kushiriki fainali hizo. Tanzania iko Kandaya Tano pamoja na timu za Eritrea, Kenya na Uganda.
Iwapo U23 itaitoa Uganda itacheza na mshindi kati ya Eritrea na Kenya. Mechi yakwanza itachezwa ugenini kati ya Juni 24-26 mwaka huu wakaya marudianoitakuwa kati ya Julai 8-10 mwaka huu.

0 maoni:
Post a Comment