Wednesday, July 6, 2011

FISH GROUP WASAKA WADHAMINI


Na Andrew Chale

KUNDI la sanaa za maigizo na filamu la Fish Group Filam linasaka wadhamini ilikuendelea kukuza vipaji vya wasanii wachanga na kuinua tasnia ya filamu nchini.
Wakiongea na mwanahabari mapema  ofisini kwao Magomeni jijini Dar es Salaam, jana viongozi wa kundi Hamis Yusuph na Juma Mwamwindi ‘Stopa’ walisema kuwa wanasaka wadhamini hao kwa kuwa mpaka sasa tayari wamesha wandaa vijana kwa kiwango kikubwa kwenye sanaa huku wengine wameokolewa kwenye makundi mabaya na kuwaweka pamoja.
“Lengo letu kukuza vipaji na kuendeleza sanaa hivyo tunaomba wadau kujitokeza na kutupa tafu ya kuendeleza gurudumu hili mpaka sasa tunajiendesha wenyewe bila wadhamini” alisema Mwamwindi ‘Stopa’.
Mpaka sasa kundi hilo linawasanii 64 na linanolewa na walimu wazoefu wakiwemo Hamad Abdala ‘Mr.Eddo na Mode ambao ni wasanii wazoefu kwenye tasnia hiyo.
Aidha waliongeza kuwa, malengo yao zaidi ni kuakikisha mbaali na sanaa ya maigizo na filamu pia wanataka kuwa na kundi la ngoma na sarakasi.
Kwa upande wake mkuu wa nidhamu wa kundi hilo, Ramadhan Shaban ‘Max well’ alisema kuwa wamepata faraja kwa wazazi wa wasanii waliojiunga na kundi hilo kuwaunga mkono kwa kuwaruhusu watoto wao kufanyaa sanaa tofauti na zamani ambapo sanaa ilionekana kama uhuni. “Tunajisikia faraja wazazi kuikubali sanaa hivyo Tanzania tunakoelekea soko litakuwa zaidi ni kushirikiana kwa pamoja



........

unaweza wasiliana nao kupitia anuani zifuatazo;0652513951 AU 0719302000 ama unaweza kufika ofisini kwao Magomeni Mapipa ,kituo cha mabasi cha Mapipa mkabala na Shibam Restaulant.





Caption Picha aliyevaa suti kiongozi wa mundi hilo, Juma Mwamwindi ‘Stopa’ akiwa na baasdhi ya wasanii wa wanaounda kundi la Fish Gruop Filam, la magomeni jijini Dar salaam

picha nyingine baadhi ya wasanii hao wakiwa kwenye picha ya pozi

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU