Mkazi wa Pongwe Tanga, Selina Anthony (kulia) akipima virusi vya ukimwi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji kuhusu ugonjwa wa HIV/AIDS iliyoandaliwa na kampuni ya Saruji Tanga katika mji wa Pongwe mkoani humo jana. Anayemtoa damu ni muuguzi kutoka katika Hospitali yaMkoa ya Bombo, Immaculata Kadaga na mtoto aliyebebwaba Selina
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Saruji Tanga, David Lee (kulia) akitolewa damu kupima virusi vya ukimwi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji kuhusu ugonjwa wa HIV/AIDS iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa wakazi wa mji wa Pongwe mkoani humo jana. Anayemtoa damu ni muuguzi kutoka katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo, Immaculata
.
: Mkazi wa Pongwe Tanga, Zainabu Hamza (kulia) akipewa ushaurinasihi kuhusu ugonjwa wa ukimwi mara baada ya kupima damu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji kuhusu ugonjwa wa HIV/AIDS iliyoandaliwa na kampuni ya Saruji Tanga katika mji wa Pongwe mkoani humo jana. Anayetoa ushauri ni muuguzi kutoka katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo, Elizabeth Lawuo. Anayeangalia ni mtoto wa Selina, Amina Adamu.





0 maoni:
Post a Comment