Mwenyekiti wa BFT Idd Kipingu akikabidhi vifaa vya michezo kwa viongozi wa BFT walivyopewa msaada na LAPF
Baraza la michezo nchini BMT, limekabidhi vifaa vya mazoezi kwa timu ya taifa ya ngumi za riadhaa kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya AFRIKA itakayofanyika nchini MSUMBIJI mwezi ujao.
Akiongea wakati wa kukabidhi vifaa hivyo vilivyotolewa na mfuko wa hifadhi ya jamii ya LAPF, mwenyekiti wa baraza hilo KANALI MSTAAFU IDD KIPINGU, ametoa wito kwa makampuni mengine kuvutiwa na hatua hiyo ili nayo yaoneshe nia ya kusaidia maendeleo ya michezo nchini
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa shirikisho la ngumi za ridhaa, BFT, MICHAEL CHANGALAWE amesema misaada hiyo itasaidia maandalizi ya timu hiyo na hatimaye kuchochea ari ya ushindani kwa mabondia kuelekea katika michuano hiyo ya AFRIKA
Miongoni mwa vifaa hivyo ni pamoja na GLOVES, PROTECTOR, PUNCHING BAGS, VIATU, TRACK SUITS, SPEED BALLS na FULANA.
Timu ya taifa ya ngumi za ridhaa inaendelea na maandalizi ya michuano ya AFRIKA, ambapo kwa sasa imeweka kambi mjini KIBAHA PWANI chini ya kocha PIMENTEL HURTADO.
0 maoni:
Post a Comment