Kushoto ni katibu mkuu wa TBF MSOFE ,katikati Afisa uhusiano wa ubalozi wa MAREKANI ROBERTO QUIROZ na makamu Rais wa TBF PHARES MAGESE kulia
Shirikisho la mpira wa kikapu TANZANIA TBF limeandaa kliniki ya mchezo huo itakayojumuisha wanafunzi wa shule ya msingi kutoka katika baadhi ya mikoa nchini ikiwa na lengo kuufundisha mchezo huo ambapo ubalozi wa marekani umefadhili mafunzo hayo kwa dola elfu kumi na tano.
Mafunzo hayo yataendeshwa na wachezaji wa zamani waliowahi kucheza katika ligi ya NBA nchini MAREKANI ambao ni TAMIKA ANDERSON,BECKY BONNER na DEE BROWN ambao wanatarajiwa kuwasili nchini tarehe 5 ambapo mafunzo hayo yaatanza tarehe 6 hadi tarehe8 katika uwanja wa DON BOSCO.
MAGESE amesema kuwa kila mkoa utatoa wachezaji 3 pamoja na kiongozi mmoja ambao watashiriki katika mafunzo hayo
0 maoni:
Post a Comment