KAMPUNI ya ujasiliamali ya Dimod Integrated Solutions & Awareness, imedhamiria kutoa semina ya siku tatu kwa wajasiliamali zaidi ya 1,000 imefahamika juzi jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Mahmoud Omar alisema semina hiyo itaanza Jumatano ijayo-Agosti 17, 2011 mpaka Ijumaa na washiriki wake watakuwa ni wananchi wa kawaida pamoja na wadau kutoka vikundi vya ujasiliamali kama vile vikoba na saccos.
Semina hiyo itafanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii kilichopo barabara ya Shekilango-Kijitonyama, jijini Dar es Salaam na “washiriki hawana budi kufika eneo la tukio kuanzia saa 8.00 asubuhi.”
Alisema kwamba kila mjasiliamali atajigharamia mwenyewe usafiri na fedha ya chakula, kadhalika atalazimika kulipa ada ya siku tatu Sh 33,000 ikiwa ni pamoja na gharama za fomu.
“Tuna programu nzito ambazo wananchi hawa watafaida katika semina hii ya siku tatu. Kwa siku zote tatu gharama au tuseme ada ni Sh 30,000 na Sh 3,000 ni kiingilio,” alisema Omar.
Alisema kwamba watafaidika kwa programu za kujitambua, namna ya kuingia sokoni, kutengeneza bidhaa kama vile vya mashambani, viwanda na mifugo.
Hadi sasa semina hiyo imepata wadhamini kama kampuni ya kupamba kumbi na sehemu mbalimbali ya Dotnatana kadhalika maduka Zizou yanayouza nguo za kisasa.
0 maoni:
Post a Comment