Wednesday, September 28, 2011

BENKI YA NBC YATOA MSAADA WA MOBILE CLINIC KWA WIZARA YA AFYA

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Lawrence Mafuru (kushoto)
akikabidhi msaada wa gari la kutolea huduma za tiba linalotembea
(mobile clinic) kwa Waziri wa Afya, Dk Haji Mponda katika viwanja vya
Karimjee jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwa Mafuru  ni Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Said Mecki Sadiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Lawrence Mafuru (kulia) akimkaribisha
Waziri wa Afya, Dk Haji Mponda katika hafla ambayo benki hiyo
ilikabidhi msaada wa  gari la kutolea huduma za tiba linalotembea
(mobile clinic) kwa Waziri huyo kwa ajili ya Bodi ya Afya Mkoa wa Dar
es Salaam jijini humo leo. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo,
Jerome Ringo na wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said
Mecki Sadiki.
Waziri wa Afya, Dk Haji Mponda akikabidhi funguo za gari la Mobile
Clinic lililotolewa msaada na benki ya NBC kwa Mwenyekiti wa Bodi ya
Afya Mkoa wa Dar es Salaam , Jerome Ringo  jijini Dar es Salaam leo.
Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Lawrence Mafuru na Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam Said Mecki Sadiki.
: Baadhi wa maofisa wa NBC na wageni waalikwa wakifuatilia kwa
makini hafla ya makabidhiano ya gari la Mobile Clinic lililotolewa
msaada na benki ya NBC kwa  Bodi ya Afya Mkoa wa Dar es Salaam katika
Viwanja vya Karimjee jijini humo
: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecki Sadiki (kushoto)
akifurahi na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Lawrence Mafuru katika hafla
ambayo benki hiyo ilikabidhi msaada wa  gari la kutolea huduma za tiba
linalotembea (mobile clinic) kwa Waziri wa Afya, Dk Haji Mponda
(hayupo pichani)  katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam
leo.
Wacheza ngoma wa kikundi cha Makumbusho Cultural Troupe wakitoa
burudani katika hafla ya makabidhiano ya gari la Mobile Clinic
lililotolewa msaada na benki ya NBC kwa  Bodi ya Afya Mkoa wa Dar es
Salaam katika Viwanja vysa Karimjee jijini humo


0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU