Monday, September 26, 2011

KILELE CHA AIRTEL RISING STARS

Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya simu ya Airtel, Rahma Mwapachu (kushoto), akimkabidhi zawadi ya kikombe, mchezaji bora wa michuano ya kukuza vipaji vya soka kwa vijana ya Airtel Rising Stars, Samil Omar wa timu ya Mkoa wa Mwanza,katika kilele cha michuano hiyo, Jumamosi Septemba 24, kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Golikipa Bora wa michuano ya kukuza vipaji vya soka kwa vijana ya Airtel Rising Stars, Denis Richard wa Mkoa wa Dar es Salaam, akikabidhiwa zawadi ya kikombe na Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya simu ya Airtel, Jane Matimbe katika kilele cha michuano hiyo, jana kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.Fainali za michuano hiyo ilishirikisha timu nne za mikoa ya Morogoro, Iringa, Mwanza na Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Leonald Thadeo (kulia), akimkabidhi nahodha wa timu ya kombaini ya vijana wa sekondari za Mkoa wa Morogoro. Charles John, kombe la ubingwa wa michuano ya kukuza vipaji vya soka kwa vijana ya Airtel Rising Stars, katika kilele cha michuano hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam jana.Katika fainali hiyo Morogoro iliyoongoza kwa pointi ilitoka sare ya bao 1-1 na Dar es Salaam.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU