Wednesday, September 28, 2011

MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KWENYE SEMINA YA TASWA MJINI MOROGORO HAYA HAPA

KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) imeteua washiriki 40 kwa ajili ya mafunzo ya waandishi wa habari za michezo yatakayofanyika mkoani Morogoro kuanzia Septemba 30, 2011 hadi Oktoba 2, 2011.

Washiriki wataondoka Dar es Salaam, Ijumaa saa 8 mchana kwa usafiri wa pamoja na watarejea Jumapili Oktoba 2, 2011 baada ya mafunzo kufungwa saa 10 alasiri.

Uteuzi umezingatia zaidi wale ambao hawakuwahi kushiriki mafunzo yoyote yaliyoandaliwa na TASWA na pia umezingatia mahitaji ya chombo husika cha habari.

Pia umezingatia mafunzo mengine yatakayofanyika Novemba mwaka huu mkoani Arusha, ambayo yatakuwa na idadi kubwa ya washiriki.

TASWA inaishukuru kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kwa kuwa mdhamini mkuu wa mafunzo haya, pia kampuni ya mabasi ya Al Saedy kwa kuwa mdhamini mwenza, tunaamini mchango wao ni mkubwa zaidi.

Mafunzo yataegemea zaidi masuala ya maadili ya uandishi wa habari, mambo ya uandishi wa makala za michezo na masuala yahusiyo sheria za michezo mbalimbali nchini.

Walioteuliwa na vyombo vyao katika mabano ni  Zaituni Kibwana (Bingwa), Olipa Assa (Dimba), Jennifer Ulembo(Mtanzania), Sweetbert Lukonge (Mwananchi), Doris Malyaga (Mwanaspoti) na Suleiman Jongo (The Citizen).

Wengine ni Renatha Msungu (Nipashe), Steve Wills (The Guardian), Maulid Kitenge (Redio One), Jimmy Tara (ITV), Master Tindwa (Capital Redio), Hassan Mvula (Star TV/Redio Free),  Alex Luambano(Clouds Media), Mbozi Katala (TBC1), na Shadrack Peter (Chanel Ten).

Pia wapo Sigori Paul (Redio Uhuru), Crecensia Tryphone (Tanzania Daima), Japhet Kazenga (Daily News), Crecence Kunambi (HabariLeo), Adolph Bruno (Majira), Shaaban Mbegu (Spotistarehe),  Shaaban Kondo (Times FM),  Hamis Shimye (Uhuru), Erasto Stanslaus (Mseto), Ezekiel Kitula (Championi), Selemani Mkangara (Changamoto), Salome Milinga(JamboLeo) na Anwar Mkama (Mlimani TV).

Wanaotoka Pwani ni Omary Mngindo na Masau Bwire, wakati wa Morogoro ni Nickson Mkilanya, Idda Mushi,Ratifa Ganzel Uhuru,  John Nditi, Abeid Dogoli,Titus Munga, Ramadhan Libenanga, Samuel Msuya, Jimmy Mengele na Lilian Lucas

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU