Timu ya taifa ya mpiwa wa pete, TAIFA QUEENS imezidi kuchanja mbuga katika michuano ya ALL AFRICA GAMES baada yah ii leo kuitandika MSUMBIJI kwa magoli 97 kwa 8
Kwa matokeo hayo TAIFA QUEENS imesonga mbele katika michuano hiyo na inakabiliana na UGANDA hapo kesho katika mchezo unaotarajia kuwa na ushindani mkubwa kutokana na wapinzani wao kuwa tishio.
Kwa mujibu wa katibu mkuu wa baraza la michezo la taifa HENRY LIHAYA aliyeko MAPUTO MSUMBIJI, amesema wawakilishi wengine wa TANZANIA kwa upande wa mchezo RIADHA wanatarajia kuanza kurusha karata zao usiku wa leo huku upande wa JUDO wakitarajia kuanza kupambana siku ya JUMATANO.
LIHAYA ameongeza kuwa timu ya taifa ya watu wenye ulemavu nayo bado haijaanza kusaka medali katika michuano hiyo kutokana na mabadiliko ya ratiba.
LIHAYA amesema timu ya CEILING nayo imeshika nafasi ya KUMI na NNE katika michuano hiyo ile hali mpaka sasa timu za soka la wanawake na ngumi zimeaga michuano hiyo
Timu ya soka ya wanawake TWIGA STARS imeyaaga mashindano hayo kufuatia sare ya kufungana mabao mawili kwa mawili na ZIMBABWE katika mchezo wa hapo jana na hivyo kufikisha pointi mbili ambazo hazitoshi kuipeleka hatua ya robo fainali.
0 maoni:
Post a Comment