Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira Duniani (FIFA) wameandaa semina ya siku tatu itakayofanyika Dar es Salaam kuanzia Oktoba 25-28, 2011 kwenye hoteli ya Peacock.
Semina hiyo inalenga kuwaleta pamoja wadau wote muhimu katika maendeleo ya mpira wa miguu kwa wanawake. Wadau wakuu ni Serikali, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, wadhamini na wanahabari.
Lengo kuu ni kutoa mwamko na kujenga uelewa zaidi wa mchango wa mpira wa miguu kwa wanawake katika jamii.
Pia kutambua nafasi na umuhimu wa wadau mbalimbali katika maendeleo ya mpira wa miguu kwa wanawake na pia kujadili na kubaini mipango, mikakati na michango mbalimbali inayotolewa/inayoweza kutolewa na wadau hao katika kumwendeleza mtoto wa kike na ushiriki wake katika mpira wa miguu.
Semina hii inalenga kujenga stadi za mawasiliano na udhamini/masoko (marketing) ili kuliwezesha shirikisho kuzitumia na kuwavutia wadhamini na wadau wengi zaidi.
Semina ya Com –Unity itatoa nafasi kwa Serikali, NGOs wadhamini na wanahabari kutoa mada mbalimbali kuhusiana na michango yao na nafasi zao katika kuendeleza mpira wa miguu kwa wanawake.
Itahitimishwa kwa Tamasha la watoto wa kike watakaocheza katika mfumo wa wachezaji watano watano Oktoba 28 mwaka huu katika viwanja vya Karume kuanzia saa tatu asubuhi. Shule zifuatazo zitashiriki;
· SOS
· Ilala Boma Shule ya Msingi
· Kurasini mahitaji maalum
· Uhuru Mchanganyiko/Uhuru Girls
· International School of Tanganyika
· Almuntazir Girls Primary School
Mchana tunatarajia kuwa na tamasha la wazazi/akina mama kutoka timu mbalimbali zitakazoshiriki. Timu hizo zitajumuisha timu ya wanakamati wa maandalizi ya Com –Unity, viongozi wa mpira wa wanawake na wanahabari toka vyombo vyetu vya habari.
FIFA itagharamia wawezeshaji, wawakilishi wake, ukumbi na vifaa vitakavyotumika na maandalizi ya Tamasha. TFF itagharamia usafiri wa ndani, gharama za ushuru na kodi na gharama nyingine.
Kamati za Maandalizi
Kutakuwa na kamati nne za maandalizi ya Semina na Tamasha. Kamati hizo ni za uratibu wa washiriki, uandaaji na uwasilishaji wa mada, udhamini na tamasha na kamati ya habari. Wenyeviti wa kamati hizo wataunda kamati kuu.
Kamati ya Uratibu wa Washiriki
• Amina Karuma– Mwenyekiti
• Michael Bundala– Katibu
• Rose Kisiwa – Mjumbe
Kamati ya Udhamini na Tamasha
• Rukia Mtingwa- Mwenyekiti
• Jimmy Kabwe- Katibu
• Devota Komba-Ikandiro – Mjumbe
• Irene Mwasanga – Mjumbe
Kamati ya Habari
• Joyce Mhaville/Deo Rweyunga- Mwenyekiti
• Boniface Wambura– Katibu
• Zena Chande – Mjumbe
• Somoe Ngitu - Mjumbe
Kamati ya Uratibu wa Uandaaji wa Mada
• Sunday Kayuni- Mwenyekiti
• Juliana Yassoda- Katibu
• Devota John – Mjumbe
• Joan Minja – Mjumbe
Kamati Kuu
• Lina Mhando – Mwenyekiti
• Devota John Marwa – Katibu
• Amina Karuma – Mjumbe
• Rukia Mtingwa – Mjumbe
• Joyce Mhaville/Deo Rweyunga - Mjumbe
• Sunday Kayuni – Mjumbe
Mshauri na Mwezeshaji wa FIFA: Henry Tandau
Tunaomba kutoa mwito kwa wadau wa mpira wa miguu wanawake watuunge mkono. Kamati ziko tayari kupokea ushauri, misaada ya hali na mali ili kufanikisha tamasha la watoto.
Lina Mhando
Mwenyekiti Kamati ya Semina ya Com-Unity
0 maoni:
Post a Comment