Na Andrew Chale
BENDI ya muziki wa dansi ya Twanga Pepeta International ‘wanakisugua kisigino’ inayotamba nchini inatarajia kuzindua albam yake ya 11 Novemba mwaka huu nchini Uingereza na Dar es Salaam.
Akizungumza mbele ya mashabiki wake waliofulika juzi usiku kwenye ukumbi wa Mango Kinondoni, muimbaji, mnenguaji na kiongozi wa bendi hiyo Ruiza Mbutu alisema kua tayari maandalizi ya ablamu hiyo yameshakamilika na mpaka mwishoni mwa mwezi ujao itakua tayari na Novemba itazinduliwa rasmi kwa mashabiki wake nchini Uingereza na jijini Dar es Salaam sambamba na Tanzania nzima.
Mbutu alikua akitanga hayo huku akiwapongeza Mkurugenzi wa bendi hiyo Asha Baraka kwa kusherekea siku yake ya kuzaliwa sambamba na mwimbaji wa bendi hiyo Haji Ramadhan aliyefanikiwa kuingia tano bora kwenye shindano la kusaka vipaji vya uimbaji Bongo star seach 2011.
“Leo ni siku ya furaha kwa wanatwanga na familia zao na furaha ya pekee ni kwa Asha Baraka amabayo leo ni siku yake ya kuzaliwa tunampongeza pamoja na Haji Ramadhan kuingia tano bora ya BSS 2011, wadau wa Twanga kwa kuwajari na kuonyesha mapenzi yetu tunarajia kutoa albam ya 11 itakayozinduliwa mwezi Novemba Uingereza nah pa Dar ” alisema Mbutu.
Katika shoo hiyo Twanga waliweza kukonga nyoyo za mashabiki wake kwa kupiga vibao vinavyotamba kutoka albamu zao mbalimbali sambamba na rapa za papo kwa papo zilizokua zikiongozwa na Muimin Mwijuma.
Kwa upande wake, Asha Baraka aliwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye bendi hiyo hasa katika vijiewe vyake kikiwemo ukumbi maalufu wa kimataifa Club Bilicanas wanapopiga shoo kila Jumatano sambamba na Jumamosi usiku ukumbini hapo pamoja na Jumapili mchana ndani ya viwanja vya Leaders Club.
MAPACHA WATATU KUINGIA MZIGONI RASMI.
VICHWA vipya kwenye maswala ya usanifu ‘graphics’ na uhariri ‘editing’ kwenye fillamu na muziki wa bongo Francis na Frank George Ntevi ambao ni mapacha wametamba kufanya kweli kwenye anga hizo ilikuleta mabadiliko ya kweli kwenye soko la filamu na muziki wa Bongo
Wakizungu na Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam, Mapacha hao walisema kua mpaka sasa wamesha fanya kazi za kuongoza na kuihariri filamu ya ‘The Magic Flower’ ya msanii na kiongozi wa shirikisho la wasanii Tanzania (TAFF)Simon Mwakifamba.
“Mpaka sasa tumesha fanikiwa kuongoza filamu ya The Magic flower ni hakika itakapoingia sokoni watanzania watakubali kiwango cha filamu na utundu uliotumika kwenye filamu hiyo” walisema Mapacha hao.
Mbali na filamu hiyo pia waliweza kufanyia graphis filamu za ‘Time after time’ iliyoigizwa na mastaa wa Bongo Izzo Bzness, Quick Raca, Jackline Wolper na filamu nyingine ni ya ‘My Angel’ part 1-2 ya Yusuph Mlela huku filamu zingine wanazozifanyia graphics na editing zipo mbioni kutoka hapo baadae.
Frank na Francis ama ‘The Squares’ wamekua wakifanya shuguli hizo za chini ya studio ya Ntevi Pro vision ya Magomeni jijini Dar es Salaam iliyo chini ya baba yao.
Mwisho









0 maoni:
Post a Comment