Tuesday, September 6, 2011

VILLA SQUAD YATAMBA KUNYWA DAMU YA MNYAMA


 
                                             Na Andrew Chale,Tanga
 
TIMU ya soka ya Villa Squad Fc 'Kambi moto' wameapa kumuangusha mnyama timu ya Simba Sc  ndani ya dakika 90 ilikuzihirisha uwezo wao katika msimu wa ligi kuu utakaochezwa kesho jumatano uwanja wa mkwakwani,TANGA
 
Akizunguma mjini hapa Katibu mkuu wa Villa, Iddy Muhsin Godigodi alisema kuwa, ana hakika na kikosi chake hicho kua kitacheza kwa hali na umoja na kuleta ushindi ndani ya dakika hizo 90,kwani timu ya Simba ni ya kawaida kama timu nyingine.
 
"Mambo yote dakika 90, sisemi sana, dakika hizo zitatosha kutupa ushindi, hivyo nawataka wachezaji wawe katika hali ya mchezo na hakika tutaendeleza wimbi la ushindi" alisema Godigodi.
 
Aidha, alisema kuwa, mpaka sasa wapo fiti na wamejiandaa na mchezo huo asilimia 100, kwa kikosi chote ambacho kitakachoshuka hiyo dimba la Mkwakwani, ambapo kipo chini ya makocha, Said Chamasi na Abdalah Msamba.
 
Kwa upande wake,Nahodha wa Villa, Shayi Mpala alisema kuwa,wachezaji wote wapo fiti na watashuka dimbani kuendeleza kichapo huku wakisema kuwa wataendelezaq ushindi huo huku wakishuka dimbani bila kuogopa majina ya wachezaji na timu."Tupo fiti hivyo dua zenu wadau wa Villa zinahitajika na hakika ushinddhidi ya Simba lazima upatikane zaidi ni dakika 90" alisema Shayi.
 
Aidha, kwa upande wa daktari wa timu hiyo, Dk Nassor Mahamoud alisema kua wachezaji wote wapo na  ila baadhi wanamaumivu kidogo ikiwemo ya enka. "wachezaji wote wanaendelea vizuri ila baadhi wana tatizo kidogo la enka, lakini si ya kuzui kucheza ila kocha ndie atajua zaidi" alisema Dak.Nassor.
 
Villa squad ipo mjini hapa toka juzi na kuweka kambi yake ambayo hata hivyo mpaka sasa ni siri kwa ukubwa wa mchezo wenyewe ipo timu nzima pamoja na viongozi waandamizi, akiwemo, mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Villa, Ally Kindoile, na wengine wengi ambao wanatarajia kutua jijini hapa leo  na kesho siku ya mch ezo wakiwemo viongozi wa na maashabik

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU