Wednesday, November 23, 2011

SAFARI LAGER YAZINDUA MPANGO WA KUWAWEZESHA WAJASIRIAMALI WADOGOWADOGO NCHINI. “WEZESHWA NA SAFARI LAGER”









Dar es Salaam, Jumatano 23, 2011: Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo Imezindua rasmi kampeni ya aina yake ya kuwatafuta na kuwawezesha wajasiriamali wadogowadogo katika shindano la wezeshwa na Safari Lager na unaweza kupata ruzuku ya kusaidia kuona njiaya mafanikio.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo alisema Bia ya safari Lager inazindua program ya wezeshwa ili kuwasaidia wamiliki wa biashara ndogondogo na za kati kukuza biashara zao,kuweza kuajiri zaidi ,kupata faida zaidi na pia kusaidia jamii yao.

Alisema program ya Wezeshwa na Safari lager itatoa ruzuku yenye thamani ya jumla ya Tsh Milioni 200 kwa kuwawezesha wafanyabiashara watakaoingia na kufuzu vigezo vya program hii.Uwezeshwaji utakuwa kwa kupewa vitendea kazi muhimu vinavyohitajika ili kukuza biashara zao.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU