SHIRIKISHO la ngumi za ridhaa nchini BFT imetaja mabondia HAMSINI watakaoanza mazoezi ya awali ya kuwania tiketi ya kushiriki mashindano ya kutafuta viwango vya kucheza mashindano ya OLYMPIKI mwakani.
Katibu mkuu wa shirikisho hilo , MAKORE MASHAGA amesema mashindano hayo ya kutafuta viwango vya kushiriki mashindano ya OLYMPIKI yamepangwa kufanyika APRIL nchini MOROCCO.
Kwa bara la Afrika, zimetolewa nafasi SITINI na SITA ambapo kati ya hizo TANZANIA inazo nafasi KUMI kama mabondia wake watakidhi vigezo vya kushiriki mashindano ya OLYMPIKI yatakayofanyika LONDON mwakani.
Mbali na kambi hiyo, pia mashindano ya taifa ambayo hushirikisha mikoa ya TANZANIA inategemewa kutumiwa kuteua mabondia wengine.





0 maoni:
Post a Comment