SHIRIKISHO la soka nchini (TFF) limetangza kuwa timu ya KILIMANJARO STARS ya TANZANIA BARA haitoshiriki katika mashindano ya kombe la MAPINDUZI lililopangwa kuanza mwanzoni mwa mwezi Januari visiwani humo.
Katibu mkuu wa TFF , ANGETILE OSIAH amesema kutokuwepo kwa timu hiyo katika mashindano hayo kunatokana na sababu kwanza ya kutokuwepo kwa makocha wa timu hiyo pamoja na suala jingine la wachezaji wa timu hiyo ambao wanaunda timu ya KILIMANJARO STARS kutoka katika vilabu VITATU vya AZAM FC , YANGA na SIMBA
Chama cha Mpira wa Miguu visiwani ZANZIBAR (ZFA), kilitoa mwaliko maalum kwa TFF kuomba timu ya KILIMANJARO STARS ishiriki katika kupamba sherehe za maadhimisho ya MIAKA 49 ya MAPINDUZI VISIWANI humo.
ZFA ilitaka TIMU ya Taifa ya TANZANIA BARA ya KILIMANJARO STARS icheze mchezo mmoja wa kufungua pazia la mashindano ya Kombe la Mapinduzi, kwa kuumana na timu ya ZANZIBAR ya ZANZIBAR HEROES.
ZFA ilitaka TIMU ya Taifa ya TANZANIA BARA ya KILIMANJARO STARS icheze mchezo mmoja wa kufungua pazia la mashindano ya Kombe la Mapinduzi, kwa kuumana na timu ya ZANZIBAR ya ZANZIBAR HEROES.
Bingwa mtetezi wa mashindano hayo ni Simba ambayo katika fainali ya mwaka huu iliwachapa wapinzani wao wa jadi, YANGA kwa magoli MAWILI kwa BILA.
Mwaka huu SIMBA, YANGA na AZAM FC ndizo timu zilizoteuliwa kushiriki mashindano hayo kwa mwaka huu yaliyopangwa kuanza Januari mbili na fainali yake kuchezwa Januari KUMI na MBILI ikiwa ni kumbukumbu ya siku ya MAPINDUZI VISIWANI.
TAIFA STARS KUCHEZA NA MISRI MECHI YA KIRAFIKI
TAIFA STARS KUCHEZA NA MISRI MECHI YA KIRAFIKI
Katika hatua nyingine Chama cha soka nchini MISRI kimeliomba shirikisho la soka nchini TFF kutaka kuchezwe mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya timu ya taifa TAIFA STARS na MISRI mwezi FEBRUARI mwakani.
Kulingana na msimamo wa ubora wa kiwango duniani, timu ya TAIFA STARS imezidi kuporomoka duniani na kufikia nafasi ya 137, wakati MISRI ikiwa katika nafasi ya THELATHINI na MOJA.
Timu ya IVORY COAST ni ya KWANZA barani Afrika na ni ya KUMI na SITA duniani kwa ubora wa viwango vya soka , ya kwanza ikiwa ni HISPANIA ikifuatiwa na UHOLANZI na ya TATU ni UJERUMANI.





0 maoni:
Post a Comment