Thursday, December 1, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WATANZANIA WAISHIO BURUNDI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati alipokutana na Watanzania waishio nchini Burundi jana Novemba 30. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Dkt. James Mwasi Nzagi (kulia) ni Mwenyekiti wa Kinamama wa Jumuiya ya Kinamama waishio Burundi, Siwajibu Hamis (wa pili kulia) ni Mwenyekiti wa Vijana wa Jumuiya hiyo, Mutalemwa Julian
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwaaga baadhi ya Watanzania waishio Burundi baada ya kumaliza mazungumzo alipokutana nao Bujumbura Burundi jana Novemba 30 na kuzungumzia mambo mbalimbali yanayoendelea katika Taifa la Tanzania
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Watanzania waishio Bujumbura Burundi, baada ya kumaliza mazungumzo baina yao yaliyofanyika jana Novemba 30 na kujadili mambo mbalimbali yanaoendelea katika Taifa la Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Makamu wa Rais wa Burundi, Therence Sinunguruza, wakati akiwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Burundi tayari kwa kuondoka nchini humo kurejea Tanzania baada ya kumaliza shughuli za Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu, uliomalizika Bunjumbura Burundi juzi Novemba 29

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU