WIZARA ya Habari, vijana, utamaduni na michezo, imesema mchakato wa kupata vazi la taifa unaendelea vizuri kwani wabunifu wazalendo wa mitindo ya mavazi nchini wameshirikishwa na kutoa mapendekezo yao.
Taarifa ya waziri wa Habari, vijana, utamaduni na michezo, DOKTA Emmanuel Nchimbi amesema ili kuhitimisha mchakato huo.
Kamati maalum ya kukamilisha mchakato huo imeundwa ambapo kamati hiyo inaongozwa na Mwenyekiti wake JOSEPH KUSAGA, katibu wake ni ANGELA NGOWI.
Wengine ni wajumbe ambao ni HABIBU GUNZE, JOYCE MHAVILLE, MUSTAFA HASSANALI, ABSALOOM KIBANDA, MAKWAIYA KUHENGA na NDESAMBUKA MERINYO.
Itakumbukwa kuwa Serikali, kupitia Idara ya Maendeleo ya Utamaduni ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, ilianzisha mchakato wa kupata Vazi la Taifa mwaka 2004.
0 maoni:
Post a Comment