Friday, January 27, 2012

MO DEWJI APOKEA MSAADA WA BAISKELI ZA WALEMAVU.

Pichani Juu na Chini ni Mh. Mohammed Dewji akipokea msaada wa Baiskeli  Tano za Walemavu kutoka kwa Mkuu wa Club za wanachama wa  Lions Club Tanzania na Uganda Satish Sharma.


Mh. Mohammed Dewji akibadilishana mawazo na baadhi wajumbe wa Lions Club. 

Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Dewji amepokea msaada wa baiskeli  5 za walemavu  kwa ajili ya jimbo lake zilizotolewa na Taasisi ya  Lions Club Tanzania.
Mh. Dewji amekabidhiwa msaada huo leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Club za wanachama wa  Lions Club Tanzania na Uganda Satish Sharma, katika makabidhiano yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Gerezani.
Mh. Dewji ameshukuru msaada huo akisema utakua faraja kwa wananchi wa jimbo lake ambao wanamatatizo ya ulemavu wa viungo.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU