Monday, February 6, 2012

AIRTEL YATOA VITABU KWA SHULE ZA SEKONDARY 4 MKOA WA MANYARA

Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Yaeda Ampa Mary Genda  na wanafunzi  wa shule hiyo wakipokea vitabu toka kwa Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde vilivyotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa shule za sekondari nne za mkoa wa Manyara ambazo ni  Yaeda Ampa, Yaeda Chii , Naberera na Merelani B.w Mkapa chini ya mpango wake wa shule yetu halfa iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii
Afisa Mahusiano wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel ,Jane Matinde akikabidhi  vitabu kwa Afisa Elimu sekondari wa wilaya ya Mbulu  Mikaeli Hadu ,kwa niaba ya shule nne za sekondari zilizokabidhiwa vitabu hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni moja kwa kila shuke,shule hizo ni  Yaeda Ampa, Yaeda Chii , Naberera na Merelani B.w Mkapa,Mkoani Manyara (katikati )ni Kaimu Mkurugenzi  Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw.Harry Sinjela
Wanafunzi , walimu ,wafanyakazi wa Airtel na viongozi mbalimbali wa halmashauri ya wilaya ya mbulu mkoani Manyara wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Airtel kukabithi vitabu kwa shule 4 za sekondari zilizopo mkoani hapa, kila shule imepata vitabu vya thamani ya shilling milioni moja.  Walikaa kutoka kushoto ni Afisa wa uhusiano wa Airtel Jane Matinde Akifatiwa na kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya mbulu  Bwana Harry Sinjela, Afisa Elimu sekondari wa wilaya ya Mbulu  Mikaeli Hadu na diwani wa kata ya Yaeda Ampa Bw Marcel Malley

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU