Mcheza Sinema maarufu toka Marekani Deidre Lorenz atashughudia mpambano wa kimataifa usio wa ubingwa baina ya Rashid “Snake Man” Matumla na bondia toka Urusi utakaofanyika katika Manispaa ya Moshi tarehe 22 Juni mwaka huu.
Deidre Lorenz amecheza sinema nyingi ikiwemo sinema maarufu ya Santorini Blue ambayo iliuzwa kwa zaidi ya dola za Kimarekani miloni 100.
Mcheza sinema huyo anayeishi katika jiji la New York (Big Apple) atashiriki kwenye mbio maarufu za Marie Frances Mt. Kilimanjaro Marathon kwa kumbukumbu ya miaka "50 ya Uhuru wa Tanganyika" zitakazofanyika katika mji wa Moshi tarehe 24 Juni. Mbio hizo zitaanzia Moshi Club mpaka Mamboleo madukani kupitia kwenye mzunguko wa YMCA.
Rashid “Snake Man” Matumla atakutana na bondia mkali wa Urusi kwenye mpambano uliopewa jina la “The Rumble on the Mountain”.
Ujio wa Deidre Lorenz unadhihirisha jinsi Tanzania hususan mlima Kilimanjaro unavyowavutia watalii wengi toka pande mbalimbali duniani. Baadhi ya sinema alizowahi kucheza ni pamoja na: Santorini Blue, The Great Fight, The Emperor's Club, Le viager (2007), Focus Room (2003), Law & Order, Special Victims Unit, Baggage, August Rush, Perfect Stranger, BelzerVizion, Copy That, El Cantante, Two Weeks Notice na nyingine nyingi.
Kutakuweko pia na mapambano mengi ya utangulizi yatakayowashirikisha mabondia wa Tanzania na wa nchi jirani hususan Pascal Bruno (TZ) dhidi ya James Kitasi (Kenya), Alibaba Ramadhani dhidi ya Sebyala Med wa Uganda, Allen Kamote dhidi ya Chalres Damas, Simom Bernard dhidi ya Saidi Yazidu na mengine mengi.
Ujio wa Deidre Lorenz ni moja ya mikakati ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa (TPBC) ikishirikiana na mashirikisho ya ngumi duniani kama IBF na CBC pamoja na majiji kadhaa hapa nchini kukuza ajira kwa vijana, kukuza utalii wa michezo (Sports Tourism) pamoja na kujenga mazingira mazurii kwa wawekezaji kuwekeza hapa Tanzania.
0 maoni:
Post a Comment