Msanii wa ngoma ya asili ya Kisukuma (jina halikupatikana) akionyesha fiisi wakati kikundi chake kilipotumbuiza katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika kijiji cha Chela wilayani Kahama Februari 25, 2012.
Askari wa Jadi yaani Sungunsu wa jimbo la Solwa wakicheza ngoma yao wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipokagua ujenzi wa hospitali ya Iselamagazi na na kuhutubia mkutano wa hadhara akiwa katika ziara ya mkoa wa Shinyanga Februari 26,2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wananchi baada ya kuwasili kwenye eneo la hospitali ya Iselamagazi kukagua ujenzi wa hospitali hiyo iliyoko jimbo la Solwa na kuhutubia mkutano wa hadhara Februari 26, 2012. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Shinyanga.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Iselamagazi katika jimbo la Solwa Shinyanga wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipohutubia mkutano wa hadahara kwenye uwanja wa hospitali ya ISelamagazi . Mheshimiwa Pinda alikuwa katika ziara ya mkoa wa Shinyanga Februari 26, 2012.
Mbunge wa Solwa Ahmed Ali Salum (mwenye kaunda suti) akisakata zeze katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye eneo la hospitali ya Iselamagazi, Shinyanga Februari 26, 2012
Mpiga zeze wa Kijiji cha Iselamagazi katika jimbo la Solwa Shinyanga (jina halikupatikana) akitumbuiza wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipokagua ujenzi wa hospitali na kuwahutubia wananchi wa kijiji hicho akiwa katika ziara ya mkoa wa Shinyanga Februari 26, 2010.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua Chuo cha VETA cha Shinyanga akiwa katika ziara ya mkoa huo, Februari 26, 2012. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Nasoro Rufunga.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua mafunzo ya ukatibu muhtasi wakati alipozindua Chuo cha VETA cha Shinyanga akiwa katika ziara ya mkoa huo Februari 26, 2012
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua mafunzo ya ushonaji wakati alipozindua Chuo cha VETA cha Shinyanga akiwa katika ziara ya mkoa huo, Februari 26,2012.
Wasanii wa ngoma ya Kisukuma ya Buyeyewakicheza ngoma hiyo wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga, Februari 26,2012.
0 maoni:
Post a Comment