1. Swali: Tunafahamu internet ya Airtel imeboreshwa, ni kwa vipi?
Jibu : Airtel imepiga hatua kubwa katika kujenga na kukuza mtandao wa technoloijia ya 3.75G Afrika kwa kuzindua rasmi mtambo wa 3.75G nchini Tanzania wenye kutoa huduma bora na yenye kasi zaidi
2. Swali: Mtambo wa data wa 3.75G ni kitu gani na mteja atafaidika na nini?
Jibu : intanet ya Airtel 3.75G inatoa huduma ya internet kwa kazi na zaidi kwa watumiaji wenye simu zenye uwezo wa kutumia internet wawapo mahali popote. Hivyo basi wateja wetu wataweza kunufaika kwa kupata huduma bora ya internet zitazowapa ufanisi katika shughuli zao za kilasiku
3. Swali: ilikupata huduma hii je nahitaji kubadili modem yangu, na je endapo tayari nilishajiunga na kifurushi tangu mwanzo nahitaji kujiunga tena ili kupata spidi ya 3.75G ?
Jibu : hakuna haja ya kubadilisha modem wala kujiunga tena katika kifurushi kingine ikiwa ulishajiunga kwa kuwa namba yako na modem vimewezeshwa mojakwamoja kupata huduma iliyoboresha kwa kupitia mitambo yetu.
4. Swali: je simu yangu isipo display/kuonyesha 3.75G inamaanisha siko kwenye mtandao huu mpya wa kasi.
Jibu : Ikiwa tayari mteja ameunganishwa na teknologia ya 3.75G simu yake itaonyesha 3.75G, HSDPA, WCDMA or HSPA. Hii inategemeana na Aina ya simu aliyonayo mtumiaji lakini kasi ya kuunganishwa ni yenye ubora zaidi.
5. Swali: Ili kupata kifurushi cha internet mteja anatakiwa kufanya nini?
Jibu : kuna malipo ya kifurushi cha Muda na ujazo, ili kupata kifurusi Muda cha siku mteja atatuma kutuma neno “datasiku” kwa kifurusi cha wiki “datawiki” na kifurushi cha mwenzi “datamwenzi” na kutuma kwenye namba 15444 na kutozwa kiwango cha vifurushi usika vyenye gharama nafuu na kuunganishwa na internet isiyokuwa na mwisho. Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti yetu ya www.airtel.com
6. Swali: Hii huduma ya 3.75G inatufikia hata wakazi wa huku mbeya na miji mbalimbali Nchini? Na ni maeneo gani mmeyafikia mpaka sasa.
Jibu : mtandao wa 3.75G umesambaa nchini katika miji 31 ambayo ni kagera, mwanza, shinyanga, Arusha, Kilimanjaro, Tabora, Singida, Manyara, Tanga, Rukwa, Dodoma, Pwani, Zanzibar, Morogoro, Iringa, Lindi na Mtwara na tumewezesha minara zaidi ya 400 nchi nzima. Huu ni mtandao mpana huduma za data za kasi zilizoenea katika maeneo mengi nchini.
7. Swali: Je unadhani huduma hii ya internet ya 3.75G itawanufaisha makundi gani na kwa jinsi gani.
Jibu : huduma hii ya internet ya kasi ya 3.75G itawafaidisha watumiaji mbalimbali ikiwemo
(i)wafanyabiashara wakubwa na wadogo katika kupata habari za biashara, kutangaza biashara zao kwenye mtandao na kuwasiliana na wateja wao
(ii) walimu na wanafunzi katika kudownload/kuperuzi kwa haraka zaidi nyenzo za kielimu za kusoma na kufundishia,
(iii)vyombo vya habari katika kutuma habari kwa njia ya picha na video ambazo zina file kubwa lakini kwa
3.75G file hizo zitaweza kutumwa kirahisi na kuongeza ufanisi. (iv)Kwa wateja wote watatumia mtandao kwenye tovuti za kijamii kama facebook, twitter, kufanya maongezi ya simu kwa njia ya video , kuangalia TV, kutuma na kupokea barua pepe na pia kupata muziki kutoka kwenye tovuti kwa kutumia simuYapo makundi mengi hayo ni machache tu.
3.75G file hizo zitaweza kutumwa kirahisi na kuongeza ufanisi. (iv)Kwa wateja wote watatumia mtandao kwenye tovuti za kijamii kama facebook, twitter, kufanya maongezi ya simu kwa njia ya video , kuangalia TV, kutuma na kupokea barua pepe na pia kupata muziki kutoka kwenye tovuti kwa kutumia simuYapo makundi mengi hayo ni machache tu.
8. Swali: Sasa mteja akipata tatizo la internet apige wapi kupata msaada wa haraka.
Jibu : Tunacho kikosi cha wafanyakazi wa huduma kwa wateja walioko kwaajili ya kuwasaidia piga 100 au tembelea maduka yetu yaliyoko nchini nzima ili upatiwe msaada na maelekezo zaidi.
9. Swali: Wateja wa Airtel na watanzania wategemee nini katika mawasiliano ya data nchini.
Jibu : Tunawaahidi wateja wetu na watanzania kwa ujumla kutegemea mapinduzi katika huduma za mawasiliano kwani tunaamini mawasiliano ndio nyenzo kuu ya shughuli za kijamii katika kukua kwa uchumi wa nchi yetu, kwa kupitia mitambo yetu iliyoenea nchini tunaendelea kuboresha huduma zetu na kuja na huduma bora za kibunifu zitazoleta ufanisi kwa watumiaji wa huduma zetu. Pamoja na 3.75G huduma ya internet ya kasi zaidi tuliyoizindua pia tumeweza kuwawezesha watanzania na kuwapatia huduma za kifedha kupitia Airtel money na kurahisisha njia za malipo, kutuma na kupokea pesa kwa wateja wetu na wadau mbalimbali. Yote hii ni katika kutimiza dhamira yetu ya kuboresha mawasiliano nchini.
0 maoni:
Post a Comment