Viingilio kwenye mechi namba 149 ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Moro United na African Lyon itakayochezwa kesho (Machi 24 mwaka huu) Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam ni sh. 1,000 kwa mzunguko na sh. 5,000 kwa jukwaa kuu.
Mwamuzi Hashim Abdallah wa Dar es Salaam ndiye atakayechezesha mechi hiyo akisaidiwa na Ephraim Ndissa na Abdallah Selega wakati mwamuzi wa akiba ni Oden Mbaga. Wote pia wanatoka Dar es Salaam. Kamishna wa mechi hiyo ni James Mhagama kutoka mkoani Ruvuma.
Pia viingilio hivyo ndivyo vinavyotumika kwa mechi zote za Ligi Kuu ya Vodacom zinazochezwa Uwanja wa Chamazi zisizohusisha timu za Simba na Yanga.
VPL itaendelea tena Machi 28 mwaka huu kwa mechi kati ya Ruvu Shooting Stars itakayocheza na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi wakati Moro United itakuwa mwenyeji wa Villa Squad katika mechi namba 153 itakayofanyika Uwanja wa Chamazi.
MTIHANI WA MAWAKALA WA WACHEZAJI
Mtihani kwa kwa ajili ya watu wanaotaka kuwa mawakala wa wachezaji na mechi wanaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Machi 31 mwaka huu saa 4 kamili asubuhi ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (FIFA).
Kwa wanaotaka uwakala huo wanatakiwa kujisajili ambapo watapewa kanuni mbalimbali za FIFA na TFF ili waweze kujiandaa kikamilifu kwa mtihani huo utakaokuwa na sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ya mtihani huo ni maswali kutoka FIFA wakati nyingine ni kutoka TFF.

0 maoni:
Post a Comment