Wednesday, March 7, 2012

AIRTEL TANZANIA YADHAMIRIA KUBORESHA HUDUMA KWA WATEJA

Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Tanzania Bi Adriana Lyamba akiongeaa na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa programme ya Airtel service Academy itakayowawezesha wafanyakazi wake kutoa huduma bora na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi, kushoto ni mkurugenzi Rasilimali watu Perece Kiringiti.
mkurugenzi Rasilimali watu wa Airtel Tanzania Perece Kiringiti akiongeaa na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa programme ya Airtel service Academy itakayowawezesha wafanyakazi wake kutoa huduma bora na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi, kushoto ni Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Adriana Lyamba.
mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Sam Ellangallor akiongeaa na wafanyakazi wa Airtel wakati uzinduzi wa programme ya Airtel service Academy  iliyofanyika leo katika Makao makuu ya Airtel Morocco.
Wafanyakazi wa Airtel pamoja na waandishi wa habari wakiwa katika uzinduzi wa programme ya Airtel service Academy itakayowawezesha wafanyakazi wake kutoa huduma bora na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi iliyofanyika katika Makao makuu ya Airtel Morocco.
Keki maalumu ya uzinduzi wa programme ya Airtel Service Academy

*        Watoa huduma 99 kuongezewa ufanisi

*        Katika siku 365
Airtel Tanzania, mtandao unaoongoza kwa gharama nafuu na wenye wigo mkubwa Tanzania leo umezindua programu ya kuwawezesha wafanyakazi wake kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kuhakikisha wateja wake wanapata huduma bora Tanzania.

Hii  inakuja baada ya ya uzinduzi mzuri wa chuo cha masoko kilichozinduliwa mwezi wa kumi mwaka jana inayojulikana kama " Airtel Centum Sales University (ACSU)"

Akiongea katika uzinduzi wa programu hii ya mafunzo kwa  timu zinazotoa huduma kwa wateja katika ofisi za Airtel ,Mkurugenzi wa Airtel Tanzania bwana Sam Elangalloor alisema,"Leo tunazindua rasmi mafunzo ya huduma kwa wateja Tanzania inayoashiria dhamira yetu katika kuleta mabadiliko na kuwaopa wateja wetu huduma bora na zenye viwango vya juu ambazo hazijawahi kupatikana Tanzania.lengo letu ni kuhakikisha tunatoa huduma ambazo zinazidi matarajio ya wateja wetu na kudumisha mahusiano ya muda mrefu.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha huduma kwa uteja, Adriana Lyamba aliongeza kwa kusema, " mafunzo haya ni muendelezo wa kuonyesha ni kwa jinsi gani kampuni na nembo yetu inajali wateja wake.Katika siku 365zijazo wafanyakazi wa Airtel katika kityengo cha huduma kwa wateja watajifunza mbinu za kitabia na zile za kikazi katika kutoa ufanisi zaidi na kuwaongezea ujuzi zaidi.

Leo Tanzania zaidi ya wafanyazi 99 wa kitengo cha huduma kwa wateja wataanza mafunzo haya ya huduma kwa wateja katika ofisi za Airtel makao makuu

Programu hii ya  Airtel service Academy inatolewa na kampuni ya ukufunzi ijulikanayo kama  Centum learning na itahakikisha watoa huduma wa Airtel wanakua bora zaidi Tanzania na Afrika kwa ujumla.
 


0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU