Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alberic Kacou (kulia) akizungumza muda mfupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani Bw. John Hendra (katikati). kushoto ni Country Representative UN Women Bi. Anna Collins-Falk.
Bw. Kacou amezungumzia tamko lilitolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la kutaka Dunia kuungana kwa pamoja katika kukomesha ukiukwaji wa haki za Wanawake Duniani.
Aidha Bw. Kacou ametoa shukrani za dhati kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Serikali ya Tanzania kwa ujumla kwa kuonyesha nia ya dhati katika kupiga vita unyanyasaji wa Wanawake ambapo amesema kwa kuonyesha mfano Rais huyo amewapa nafasi za uongozi na kusema kuwa Wanawake wakiwezeshwa wanaweza.
Assistant Secretary-General, Deputy Executive Director for Policy and Programme wa Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa John Hendra (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alberic Kacou na kushoto ni Country Representative UN Women Bi. Anna Collins-Falk.
Katika Hotuba yake Bw. Hendra ameelezea mikakati ya Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha siku hiyo ikiwemo tukio la kupanda Mlima Kilimanjaro lenye kauli mbiu “Climb Up- Speak Out” ikiwa ni katika jitihada za kupamba na ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa kike.
Baadhi ya waandishi wa habari na maafisa wa Umoja wa Mataifa wakifuatilia kwa makini hotuba zilizokuwa zikitolewa wakati wa maadhimisho ya UN ya Siku ya Wanawake Duniani leo.
Umoja wa Mataifa kwa kupitia Shirika lake la wanawake leo umeadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani kwa kutoa wito kwa jamii kushirikiana kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake.
Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam leo, Assistant Secretary-General, Deputy Executive Director for Policy and Programme wa Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa John Hendra amesema Umoja wa Mataifa unaunga mkono juhudi za Tanzania katika kukabiliana na ukiukwaji wa haki za mtoto wa kike na wanawake kwa ujumla.
Awali akimkaribisha Bw. Hendra, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bw. Alberic Kacou amesema Umoja wa Mataifa unafanya kazi bega kwa began a serikali ya Tanzania katika kufanikisha utekelezaji wa sera ya haki na usawa kwa wanawake na wanaume.
0 maoni:
Post a Comment