Thursday, March 29, 2012

UN YAADHIMISH​A KUMBUKUMBU YA WAHANGA WA BIASHARA YA WATUMWA KWA KUTOA ELIMU KWA WANAFUNZI.

Bi. Harriet Macha kutoka Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) akifafanua lengo la ziara hiyo ambapo amesema ni muhimu kwa wanafunzi na vizazi vijavyo kujua historia na madhara yaliyotokana biashara ya utumwa. Katika kuadhimisha kumbukumbu ya biashara ya utumwa duniani Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa kimegharamia ziara ya wanafunzi kutoka shule tatu jijini Dar es Salaam kwenda kutembelea kituo cha Kihistoria cha Kaole kilichopo Bagamoyo.
 Mtaalamu wa Mambo ya Kale Bw. Jumanne Majige akitoa maelezo kwa wanafunzi
 Wanafunzi wakishangaa kisima cha maajabu. Ksima hicho kiliaminika kuwa cha maajabu baada Serikali kuwahi kuchota takribani Lita 10,000 za maji lakini kiwango cha maji hayo hakikupungua.
Wanafunzi wakinawa maji ya katika kisima cha maajbu kwa imani ya kuwa ni yenye baraka. Kisima hichi hakikauki maji wala kuongezeka tangu enzi za ukoloni na kinaaminika kuwa ni cha maajabu.
  Bw. Jumanne Majige akitoa maelezo kwa wanafunzi kuhusu Kaburi la wapendanao waliokufa siku moja kwenye bahari ya Hindi na kuzikwa pamoja lililopo Kaole Bagamoyo.
Mti wa Mbuyu unaosadikiwa kuwa na miaka 500.
Stella Vuzo kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa akizungumza na waanafunzi kutoka shule za Benjamini Mkapa, Kibasila, Lugalo na  Mbezi . Katika mazungumzo hayo akizungumzia lengo la Umoja wa Mataifa kuwa ni pamoja na kuhakishasha biashara ya Utumwa inatokomezwa kabisa na kuwaasa vijana wajijengee utamaduni wa kusoma vitabu na kuzijua haki zao za msingi na kujitambua.

Bi. Vuzo alitoa changamoto hizo katika ziara hiyo ambapo pia alitoa fursa hiyo kuwasilisha ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliutoa katika maadhimisho ya siku ya kuwakumbuka wahanga wa biashara ya utumwa duniani inayodhimishwa kila mwaka tarehe 25 mwezi Machi.
Kiongozi wa msafara kutoka Kitengo cha Umoja wa Mataifa Bi. Stella Vuzo akibadilishana mawazo na Mwanafunzi Nuru wa Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa. Kwapicha zaidi Bofya hapa

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU