Monday, March 5, 2012

CHAMA CHA MPIRA WA PETE NCHINI (CHANETA) KIMEONGEZA WACHEZAJI SABA

 
Kaimu katibu mkuu Rose Mkisi
 
Chama cha  mpira wa pete nchini (CHANETA) kimeongezawachezaji saba  wanaotakakujiunga na timu ya taifa TAIFA QUEEN inayojiandaa na michuano ya kombe la AFRIKA itakayofanyika mwezi  MEI mwaka huu nchini TANZANIA.

Kaimu  katibu mkuu wa CHANETA ROSE MKISI amesema kuwa wachezaji hao wamechaguliwa kutoka katika  baadhi ya timu zilizoshiriki ligi daraja la pili mwaka huu na wameonyesha viwango vikubwa wakati wa mashindano.
MKISI amewataja wachezaji hao ni pamoja FROLIA PASCALIA kutoka Wizara ya maendeleo ya jamii,MATALENA MHAGAMA kutoka BANDARI ,NIPAEL KESSY  na MPARA IDDI wote kutoka JESHI STARS, ADELA CHRISTOPHER wa timu ya POLISI na PENINA MAYUNGA anayechezea timu ya JKT RUVU.

Wachezaji hao tayari wamepewa barua za kufahamishwa kuhusiana na uteuzi huo ambapo watajiunga kambini na wachezaji wenzao hivi karibuni kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya AFRIKA.

Wachezaji hao watachujwa kulingana na uwezo wao wakati wa kambi ambapo wachezaji wanaotakiwa na kumi na sita watakaoshiriki mashindano ya AFRIKA.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU